Connect with us

Makala

PSG,Tutaendeleza Ligi Nje Ya Ufaransa

PSG imesema kuwa itacheza michezo yake ya Ligi ya mabingwa Ulaya nje ya Ufaransa kwa kuwa nchi hiyo imezuia michezo hadi Septemba kutokana na virusi vya Corona ambavyo vimesambaa duniani kote.

PSG walikuwa wameshafuzu kwa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na sasa walitakiwa kucheza michezo miwili tu nyumbani ili wafuzu kwa fainali hivyo wataendelea kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ligi kuu ya Ufaransa kusitishwa hadi mwezi September.

Mwenyekiti wa PSG, Nasser Al-Khelaifi amesema kuwa wanaiheshimu nchi yao kutokana na tamko hilo watakwenda kucheza michezo yao nje ya Ufaransa.

“Tunaheshimu maamuzi ya nchi yetu na sasa tutacheza michezo yetu nje ya Ufaransa, tunasubiri kuona UEFA watasema nini lakini naamini kuwa bado tutaendelea na michezo yetu kama kawaida,” alisema Nasser Al-Khelaifi.

Uefa wanaamini michezo ya Ligi ya mabingwa Ulaya itaendelea tena mwezi Agosti mwaka huu ikiwa janga la Corona Virus litapungua duniani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala