Connect with us

Makala

Psg,Man Utd Vitani Kumuwania Ndindi

Manchester United imeingia vitani na Paris Saint German kuwania saini ya mchezaji wa Leicester City ,Wilferd  Ndindi ambaye ni kiungo tegemeo kwenye klabu yake hata kuwavutia miamba hiyo ya Ulaya kutokana na kucheza kwa kiwango kizuri msimu huu.

Ndindi ana mchango mkubwa kwenye klabu hiyo inayojiita pia King Power ,ambao msimu huu wanakula sahani moja na vigogo kwenye msimamo wa ligi kuu England wakishika nafasi ya tatu.

Nyota huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2024 kwa kununuliwa na Leicester City kwa pauni 17 mil kutoka Genk ya Ubelgiji,amecheza jumla ya mechi 23 kati ya 27 ambazo klabu yake imecheza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala