Connect with us

Makala

Pogba Kuzua Balaa Ulaya

Inter Milan imeingia kwenye bato la timu nne zinazopambana kumng’oa Paulo Pogba huko Manchester United kwenye usajili wa msimu ujao.

Nyota huyo Mfaransa anaonekana kuwa mguu ndani nje Man United hasa baada ya mwenyewe kukiri kutaka kwenda kutafuta changamoto mpya kwingineko.

Kocha wa Real Madrid,Zinedine Zidane kwa muda mrefu amekuwa akimtaka kiungo huyo anayeshikilia rekodi ya kusajiliwa kwa pesa nyingi ligi kuu England  lakini kuna mpango pia wa kiungo huyo kurudi Juventus mahali ambapo alishatamba  kwa miaka 4 kuanzia 2012/2016.

Paris Saint-Germain pia wanataka kuinasa saini ya nyota huyo ili kucheza ndani ya Ufaransa ikiwa ni baada ya kuwauza  Neymar ndani ya Barcelona.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala