Connect with us

Makala

Penalti Yawapeleka Simba Robo Fainali

Hatimaye kikosi cha Simba Sc kimetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kupata ushindi wa penalti 3-2 mbele ya Stand United katika uwanja wa Kambarage kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.

Hassan Dilunga kwa mkwaju wa penalti alifunga bao la kwanza dakika ya 51 lililosawazishwa na Stand United dakika ya 67 kupitia Miraji Saleh.

Kwa upande wa Simba penalti zilifungwa na Clatous Chama, Deo Kanda na Hassan Dilunga huku Meddie Kagere na Ibrarahim Ajibu wakikosa penalti zao.

Licha ya Stand United inayoshiriki Ligi daraja la kwanza kumaliza mpira ikiwa pungufu kufuatia mchezaji wao Mwente kuonyeshwa kadi nyekundu ilifunga mabao mawili kupitia kwa Brown Raphael na Juma Ndaki.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala