Connect with us

Makala

Mwakalebela Asalimu Amri Kwa Senzo

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela ameomba radhi klabu ya Simba, Yanga, TFF na mashabiki wote wa soka kufuatia kauli aliyoitoa jana.

Jana Mwakalebela alisikika akisema yupo kwenye mazungumzo na mchezaji wa Simba Clatous Chama kwa ajili ya mipango ya kumsajili ili ajiunge na Yanga.

Mwakalebela anasema alisema amefanya mazungumzo na Chama kuhusu uwezekano wa kumsajili kwa lengo la utani kwa sababu hivi karibuni Simba walikuwa wanatamba watamsajili Tshishimbi lakini mapokeo yamekuwa tofauti.

“Nachukua nafasi hii kuelezea hali ambayo naona imezua sintofaham kwa suala ambalo nilizungumzia na mchezaji wa Simba Clatous Chama ambapo inaelekea Simba hawajalipokea vizuri jambo hili”- AlisemaFredrick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga.

“Kwanza natumia fursa hii kuomba msamaha kwa klabu ya Simba na wapenzi wa Yanga. Kama ambavyo tulikuwa tunaona na kusikia wenzetu wa Simba wakitutania kuhusu mchezaji wetu Papy Tshishimbi, basi na mimi nikaona huu ni utani wa jadi na mimi naweza kuzungumza jambo.”

“Kiukweli na uhalisia mchezaji huyo (Chama) sijazungumza nae lakini kama kungekuwa na haja ya kuzungumza nae mimi kama kiongozi wa juu mwenye weledi katika soka, ningetumia utaratibu kwa sababu nafahamu utaratibu.”

“Kwa kuwa hapa katikati tumekuwa na mazungumzo ya utani kati yetu na wenzetu wa Simba hata ukiangalia kwenye mitandao ya kijamii walikuwa wakieleza kuwachukua wachezaji wetu kama Tshishimbi basi na mimi nikaona niseme jambo.”

“Inaonekana jambo hili nimelizungumza limevuka mipaka basi natumia fursa hii kuiomba msamaha Simba, TFF na wenzangu wa Yanga. Labda nilizidisha utani naamini kabisa jambo kama hili halitaweza kutokea tena kwangu. Naomba jambo hili liishe turudi kwenye undugu wetu na tuendelee na utani wetu ambao hautavuka mipaka.

Cc:Shaffihdauda

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala