Connect with us

Makala

Mugalu,Onyango Hatihati Kuwavaa Polisi

Mastaa Chrispine Mugalu na Joash Onyango wana hatihati ya kushiriki katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania utakaofanyika kesho katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Mastaa hao walikua wakisumbuliwa na majeraha hali iliyowapelekea kukosa mchezo wa kuwania kufuzu klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Plateau United ya nchini Nigeria mchezo ambayo Simba sc ilifanikiwa kufuzu baada ya matokeo ya ushindi ugenini na Sare hapa nyumbani.

“Chris Mugalu yuko vizuri baada ya majeruhi na Joash Onyango amerudi baada ya kupata majeraha akiwa Nigeria na kuna uwezekano kesho wakacheza lakini uhakika zaidi ni mchezo wa jumapili’Alisema kocha Sven Vandebroek huku pia akithibitisha kukosekana kwa Rally Bwallya mwenye matatizo ya kifamilia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala