Connect with us

Makala

Mtihani Mzito kwa Samatta Ni Huu

Supastaa wa Tanzania, Mbwana Samatta atakuwa na shughuli nzito kesho ya Kukiongoza kikosi  cha ushambuliaji wa Aston Villa kukabiliana na Manchester  City chini ya kocha wake muhispaniola ,Pep Guardiola kwenye kipute cha fainali ya kombe la ligi huko Wembley.

Katika fainali hiyo ya ligi zawadi nono itatolewa ikiwa ni pauni 100,000 kwa mshindi wa kwanza na pauni 50,000 kwa mshindi wa pili.

Mechi hii itakuwa ya kwanza kwa Samatta kucheza huko Wembley akiweka rekodi ya mtanzania wa kwanza kucheza kwenye uwanja huo wenye hadi kubwa huko Ulaya.

Kazi ni kwake Samatta kuipa Aston Villa taji na pauni 100,000 au kuishia kuvaa medali ya kuwa washindi wa pili na mkwanja wa pauni 50,000.

Kila kitu kitaangaliwa kwenye mchezo huu licha ya Aston kupoteza katika mechi tatu zilizopita ambapo walipiwa na Bournemouth,Tottenham Hotspur na Southampton huku Manchester City wakishinda mechi zote tatu zilizopita mbele ya West Ham United, Leicester City na Real madrid.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala