Connect with us

Makala

Mourinho Atamani Bale Arejee Uwanjani

Kocha mkuu wa Tottenhum Hotspurs,Jose Mourinho amekiri kutokuwa na uhakika kuhusu wakati ambapo sajili mpya Gareth Bale atarejea uwanjani kusakata soka, lakini amesema anatamani mno kumpa nafasi nyota huyo nafasi ya kudhihirisha ukubwa wa uwezo wake.

Raia huyo wa Wales alijiunga upya na Spurs kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka Real Madrid mnamo Septemba 19, 2020.

Bale aliagana na Spurs mnamo 2013 baada ya kusajiliwa na Real kwa kima cha Sh11 bilioni na akiwa RealMadrid, alifunga zaidi ya mabao 100 na kusaidia kikosi hicho kutwaa mataji manne ya klabu bingwa Ulaya (UEFA).

Kwa mujibu wa Spurs, Bale alijiunga nao akiwa na jeraha la goti alilolipata wakati akichezea Wales mwanzoni mwa Septemba 2020 na daktari wao alimpokea na kutoa ripoti kuwa nyota huyo atakosa michuano ya Spurs dhidi ya Shkendija katika pambano la Europa League, Newcastle United na baadaye Manchester United.

Endapo ubashiri wa klabu utatimia, basi Bale huenda akarejea kutambisha waajiri wake dhidi ya West Ham United mnamo Octoba 17, mechi ambayo itafuatwa na nyingine dhidi ya Burnley halafu Brighto

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala