Connect with us

Makala

Morrison Pasua Kichwa

Mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison leo ametumia dakika 64 ndani ya Uwanja wa Taifa akidhibitiwa na mabeki wa safu ya Simba iliyokuwa ikiongozwa na Pascal Wawa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali.

Morriosn baada ya kutolewa kwenye mchezo aligoma kukaa benchi na wachezaji wenzake jambo ambalo lilizua tahamaki licha ya kurudishwa na mwamuzi wa nje hakutaka kufanya hivyo zaidi ya kuongeza mwendo kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Kagera Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Kufungwa kwa Yanga mbele ya Simba kwa mabao 4-1 imewapa tiketi Simba Sc ya kusonga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo watacheza na Namungo FC  ya Lind katika Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala