Connect with us

Makala

Mghana Awapasua Kichwa Arsenal

Atletico Madrid wanaimani ya kumpamkataba mpya kiungo wao mkabaji ,Thomas Partey ambaye yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na kocha wa Arsenal ,Mikel Arteta.

Msimu wa hivi karibuni kabla ya kusimamishwa kwa ligi kuu ili kupambana na virusi vya Corona ,Arsenal imekuwa ikiruhusu mabao na kutoonyesha mashambulizi ndiyo maana Arteta anaamini kupatikana kwa mghana huyo kutabadili timu yake baada ya kung’ara misimu mitatu chini ya Diego Simeone.

Partey alikuwa nyota wa mchezo katika mchezo wa nyumbani na ugenini dhidi ya Liverpool katika hatua ya 16 bora ligi ya mabingwa Ulaya.

Nyota huyo anaruhusiwa kuachiwa kwa kipengele cha pauni za Uingereza milioni 43 (bilioni 107) ambazo zinaripotiwa kuwasilishwa kutoka Italia wiki iliyopita na Arsenal.

Lakini Atletico wanahaha kumfunga na mkataba mpya kiungo huyo wa miaka 26 huku mazungumzo yakiwa yameshaanza kitu ambacho kitafanya dau ya kipengele hicho kupanda hata kama mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2023.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala