Connect with us

Makala

Messi aondoka rasmi Barcelona

Klabu ya soka ya Barcelona imetangaza rasmi kuwa mshambuliaji na nahodha wa timu hiyo na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi hatosalia tena kwenye klabu hiyo kutokana na vikwazo vya kiuchumi na kikanuni vya ligi hiyo.

Messi amekuwa mchezaji huru tanagu Julai mosi mwaka huu pindi mkataba wake ullipoisha.

Barcelona na Messi walishakubaliana maslahi na mkataba mpya na hata kufikia kupunguza mshahara wake kwa asilimia 50 lakini kanuni za La Liga ziliwataka kupunguza mishahara na kuuza baadhi ya wachezaji kuendana na kanuni zao.Pande zote mbili zimesikitishwa kutokana na kushindwa kutimiza matamanio yao ya kuendelea kufanya kazi pamoja.

Klabu hiyo imemshukuru Mchezaji huyo kuhudumu kwa miaka 21 na imemtakia kila la kheri katika maisha yake ya soka na binafsi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala