Connect with us

Makala

Mbeligiji Kumrithi Zahera

Klabu ya Yanga sc ipo mbioni kumshusha kocha Luc Aymael raia wa ubeligiji kuja kuifundisha timu hiyo akichukua nafasi ya Mkongo Mwinyi Zahera aliyetimuliwa klabuni hapo.

Kocha huyo anakuja kuchukua nafasi hiyo ambayo ilikua ikikaimiwa na Bonifasi Mkwasa kwa miezi takribani miwili ambaye alikua akisaidiwa na Said Maulid.

Taarifa zinaeleza kocha huyo mpya ni kocha mwenye uzoefu wa soka la Afrika akifundisha soka katika vilabu vya AS Vita, AFC Leopard, Rayon Sports, Al Nasr, El – Merreikh, Polokwane na Black Leopard.

Licha ya kufundisha vilabu hivyo pia alitwaa makombe mbali mbali kama ifuatavyo:

1. League championship DR Congo akiwa na AS Vita Club (2010),

2. Gabon akiwa na Missile FC (2012).

3.Pia alishinda National Super cup nchini DRC akiwa na AS Vita Club(2011),

4. National cup akiwa na AFC Leopards Kenya (2013),

5. Alishinda kombe la  South African Nedbank cup na  Free State Stars (2018),

6. Alishinda Ke Yona Nebbank Super cup 2018

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala