Connect with us

Makala

Mbelgiji Awekwa Kitimoto Yanga.

Mabingwa wa kihistoria Yanga wamemleta kocha mpya Luc Eymael kutoka Ubelgiji nchini Januari 9 ambapo alitua saa tisa alasiri na kuunganishwa moja kwa moja Zanzibar kutazama vijana wake.

Luc Eymael amepewa wakati mgumu kwa sasa baada ya kuwekwa kitimoto cha kusaini mkataba wa miezi sita kwa ajili ya kutazamiwa kama anaweza kuirudisha Yanga ya 1935.

Bodi ya Yanga imeweka bayana mkataba huo kuanza rasmi Jumatano 15 ,ambapo Yanga vs Kagera Sugar watacheza katika uwanja wa Taifa saa moja jioni.

Kocha huyo hakuwa na lakusema ila kuhitaji majina ya wachezaji wanne kwanza ili atazame maendeleo yao,na kujua wapi pakuanzia.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala