Connect with us

Makala

Manchester United Yawafunga Wolves

Mchezaji wa Manchester United Juan Mata ameiongoza timu hiyo kuwafunga bao 1-0 Wolves katika mchezo uliochezwa hapo Januari 15 katika uwanja wa Old Trafford.

Bao hilo lilifungwa dakika ya 67 na kudumu katika kipindi chote cha mchezo japo kwa upande wa Manchester United wachezaji wawili walipewa kadi za njano akiwemo Fred dakika ya 37 na Harry Magure dakika ya 59 kwa kuwachezea faulo wachezaji wa Wolves.

Wolves nao hawakuachwa nyuma kupewa kadi za njano kwa wachezaji wawili ambao ni Pedro Neto dakika ya 74 na dakika ya 89 Leander Dendonker.

Ushindi huo unawapa nguvu Manchester United ya kujiamini kuelekea mchezo wake wa ligi kuu England dhidi ya timu iliyo nafasi ya kwanza Liverpool ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 21  siku ya Jumapili licha ya kuumia kwa mshambuliaji wa United Macus Rashford.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala