Connect with us

Makala

Manara Atetea Kauli Yake

Mkuu wakitengo cha habari klabu ya Simba sc ametetea kauli yake ya kutaka mashabiki wa Simba sc wajae uwanjani siku ya jumamosi akiwa na lengo la kuleta hamasa si vingine.

Manara amesema kauli yake ya kutotaka mashabiki wa klabu zingine haikua na lengo la kuleta vurugu bali ni kahamasisha mashabiki wa klabu yake wajae maana tiketi elfu 30 ni chache zaidi kwa mashabiki wa klabu hiyo.

“Nafasi 30,000 hazitutoshi Simba kwa kuwa tuko wengi, ndio maana nilitaka waje Simba wengi kushangilia. Nafikiri kuna watu hawakunielewa makusudi au bahati mbaya.

“Ndio maana nimejitokeza na kusema tuwafundishe Yanga ustaarabu, kama ikitokea shabiki wetu ameingia tusilipe kisasi, lazima tuendeleze ule utamaduni wetu wa kujali na upendo kwa kila shabiki bila kubagua.

“Mashabiki wa Simba wamepigwa dhidi ya Azam, wamepigwa dhidi ya Mtibwa na wako ambao hawakusema. Sasa mashabiki wa Simba, wawafundishe hawa kwa ustaarabu,” amesema.

Manara wakati akiongea na waandishi wa habari alitoa kauli iliyotafasiriwa kuwa ya kibaguzi wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu mchezo huo wa klabu bingwa baina ya Simba sc na Plateau United siku ya jumatano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala