Connect with us

Makala

Madrid Mabingwa SuperCup

Klabu ya Real Madrid imefanikiwa kutwaa taji lake la kwanza kwa msimu huu baada ya kuifunga Atlanta Fc ya Italia 2-0 katika mchezo wa fainali wa kombe la Super Cup uliofanyika katika jiji la Warsaw nchini Poland.

Madrid ikianza mchezo huo na full kikosi kilichosheheni mastaa wake wakubwa wakiwemo Kylian Mbappe,Vinicius Jr na Rodrygo Goes ilitawala mchezo huo kwa dakika zote 90.

Atlantic pamoja na kujitahidi kushambulia kwa kushtukiza walijikuta wanajisahau na kufungwa bao la kwanza na Federicko Ververde dakika ya 59 akimalizia pasi ya Vinicius Jr ambayo aliwalaghai mabeki wa timu hiyo na kuwazidi maarifa na kutoa pasi hiyo kwa mfungaji.

Kylian Mbappe alifunga bao lake la kwanza kwa Real Madrid dakika ya 68 na kuzua shangwe kwa mashabiki wa Real Madrid huju bao hilo likidumu mpaka mwisho wa mchezo ambapo Madrid walikabidhiwa taji hilo la kwanza na la nne kwa mwaka 2024.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala