Connect with us

Makala

Mabondia 20 Kuchujwa Mwanza

Siku ya kesho Jumamosi mabondia 20 watazichapa katika pambano la kuwapata mabondia nane watakaoiwakilisha Mwanza kwenye mashindano ya ngumi za ridhaa Taifa tarehe 25 March mkoani Tanga.

Jopo la makocha wamejiandaa vyema kuchagua mabondia wazuri watakaowachuja na kuwaingiza kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo ya kuuwakilisha mkoa wa Mwanza.

Katibu wa chama cha ngumi za ridhaa wilaya ya Nyamagana ,Hamad Mabula amesema kuwa pambano hilo litafanyika  ukumbi wa Bundasliga uliopo eneo la Nyasaka na mabondia wote wameshakamilisha kupima uzito pamoja na afya zao tayari kabisa kwa pambano hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala