Connect with us

Makala

Mabilioni Ya GSM Yamfanya Mo Kuongea

Bilionea wa Simba Sc, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameanza kutoa maneno  kwa matajiri wa Yanga na kampuni ya GSM iliyomtengea mamilioni kiungo wake Hassan Dilunga ili kuhakikisha anatua Jangwani.

GSM hivi karibuni wapo kwenye mpango wa kumpeleka kiungo huyo Jangwani kwa dau la sh mil 80 kwani ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu akiwepo na Deo Kanda ambaye naye yupo kwenye mipango ya usajili Yanga.

Kutoka ndani ya kamati ya utendaji wa Simba Sc ,mwekezaji wa klabu hiyo ambaye ni Mo ,amesema hatakubali kumuachia mchezaji yeyote muhimu na tayari ameshaanza mazungumzo na wachezaji hao huku akiwaahidi kuwapatia dau zito kila mmoja wanalotaka ili wasitue yanga.

Mo aliongeza kuwa amepanga kuwabakisha wachezaji wote ambao mkataba wao unakaribia kumeguka kwani wachezaji hao wote wapo kwenye mapendekezo ya ripoti ya kocha Mbelgiji ,Sven Vandenbroeck aliyoikabidhi  kwenye kamati ya usajili wa timu hiyo.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala