Connect with us

Makala

Luis,Niyonzima Wajifungia Ndani

Luis Miqquisone ambaye ni kinara wa Simba Sc na Haruna Niyonzima wa Yanga Sc wameamua kujifungia ndani tangu ligi kuu isimamishwe kutokana na kujikinga na virusi vya Corona.

Kwa upande wa Niyonzima ameamua kujikinga na ugonjwa wa virusi kwa kukaa ndani hata kutosogeleana na majirani zake kwani mkusanyiko na kugusana ni moja ya maambukizo hayo.

“Nimeamua kukaa ndani  muda wote ili kukwepa mikusanyiko ya watu ikiwa ni chanzo cha kimojawapo cha ugonjwa huu hatari”alisema Niyonzima.

Luisi wa Simba alisema hakuweza kutoka nje ya geti tangu alipotoka mazoezini siku ya jumatatu amekuwa mtu wa kujifungia kwenye nyumba yake na kutoruhusu muingiliano wa mtu yoyote ndani ya nyumba yake.

“Nafanya hivi kwa ajili ya kujikinga na virusi hivi hatari vya Corona,hata nikitaka vocha nanunua kupitia simu  pia chakula ,maji na vitu vingine nilishaweka kwa wingi ndani kwangu na ninachokifanya kwa sasa ni kutumia”alisema Luis

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala