Connect with us

Makala

Liverpool Wabeba Ndoo Super Cup

Mambo bado hayajakaa sawa kwa Frank Lampard baada ya jana kushuhudia kikosi chake kikiangamia kwa magoli 5-4 dhidi ya Liverpool katika hatua ya matuta baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika dakika tisini za mchezo huo uliochezeshwa na marefa watatu wa kike.

Iliwachukua Chelsea dakika 40 kupata goli la kwanza likifungwa na Oliver Giroud huku Liverpool wakisawazisha kupitia kwa Sadio Mane mapema kipindi cha pili mabao yaliyodumu mpaka dakika tisini za mchezo huku Sadio Mane akiongeza goli la pili ndani ta dakika za mwanzoni baada ya dakika 30 kuongezwa goli lilisawazishwa na Joginho kwa mkwaju wa penati baada ya kipa wa Liverpool Adrian kucheza faulo ndani ya boxi la mita 18.

Mchezo ulimalizika kwa hatua ya matuta ambapo shujaa alikua kipa wa Adrian baada ya kucheza Penati ya kinda Abraham huku kwa upande wa liverpool Firmino,Fabinho,Origi,Alexander-Anord na Salah wakipata penati zao.

Kombe hili limewafanya liverpool wafikishe jumla ya makombe 43 katika historia yao ya mataji kwa ujumla na kuwazidi mahasimu wao wakuu wa uingereza Manchester united kwa kombe moja wakiwa na mataji 43.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala