Connect with us

Makala

Ligi Kuu Kuchezwa Bila Mashabiki-Azam Fc

Ofisa Habari wa Azam FC ,Thabit Zakaria amesema kuwa hakuna tatizo iwapo Ligi Kuu Bara itarejea na kuchezwa bila mashabiki kwa kuwa imetokea ikiwa ni dharula kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa imesema kuwa kuna uwezekano ligi ikarejea Juni ila Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa itachezwa bila mashabiki pia watategemea kauli ya Serikali.

“Kucheza ligi bila mashabiki hiyo ni kama dharula imetokea hakuna namna ya kupinga kwa sasa ni sawa ukiwa vitani huchagui silaha kikubwa ni kupambana ila cha msingi mashabiki watulie nyumbani watapata taarifa kupitia vyombo vya habari,” alisema Thabit

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 54 kibindoni baada ya kucheza mechi 28.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala