Connect with us

Makala

Ligi Kuu Bara Mchaka Mchaka

Ligi kuu ya soka Tanzania bara inaendelea tena jioni ya leo kwa michezo mbalimbali ambayo itafanyika katika viwanja tofautitofauti nchini.

Singida United watawakaribisha Alliance mchezo utakaofanyika katika uwanja wa Namfua huku wakikumbuka sare waliyoipata dhidi ya mbao fc uwanjani hapo katika mchezo uliopita ambapo safu ya ushambuliaji wa klabu hiyo ilishindwa kubadili matokeo kutokana na kukosa nafasi za wazi.

Mbao watasafiri mpaka mjini Shinyanga kuwafata Mwadui huku wakikumbuka sare waliyoipata dhidi ya Singida united ugenini hivyo leo hawana budi kutafuta ushindi mbele wa Mwadui mchezo utakaofanyika katika uwanja wa Mwadui complex.

Selemani Matola ataiongoza Polisi Tanzania kucheza ugenini dhidi ya Ruvu Shooting mchezo utakaofanyika katika uwanja wa mabatini ambapo Ruvu wanakumbuka kulazimishwa sare na Coastal union uwanjani hapo wiki iliyoisha.

Simba sc imesimama kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 9 baada ya kushinda michezo mitatu iliyocheza mpaka sasa huku kagera wakiwa nafasi ya pili wakifanana pointi na Simba lakini wakiwa na wastani tofauti ya mabao ya kushinda na kufungwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala