Connect with us

Makala

Diogo Jota Anukia Lazio

Lazio ina mpango wa kuimarisha kikosi msimu ujao kwa kumnyakua staika wa Wolverhampton Wanders,Diogo Jota ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ureno .

Nyota huyo anaweza kujiunga na klabu hiyo ya Serie A endapo Biancoceleste kama inavyofahamika itafuzu kucheza ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao.

Jota kwa sasa ana umri wa miaka 23 pia ana mkataba na Wolves unaomalizika June 2022 huku tayari akiwa amefunga mabao 6 na kutengeneza pasi 7 katika mechi 25 za ligi.

Msimu uliopita Lazio iliwauzia Wolves wachezaji wawili kutoka Ureno ,Pedro Neto na Bruno Jordao hivyo kutokana na uhusiano wao wa karibu na wakala wa Jota,Jorge Mendes unaweza ukarahisisha dili hilo.

Lazio kwa sasa ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikizidiwa pointi moja na Juventus kabla ya msimu kusimamishwa kutokana na kupambana na virusi vya Corona.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala