Connect with us

Makala

Lamine Yanga Kuikosa Tanzania Prisons

Beki wa Yanga Sc,Lamine Moro ana hatihati ya kukosa mchezo wa Septemba,6 dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa majira ya saa 1:00 usiku uwanja wa Mkapa kutokana na jeraha la goti alilolipata akiwa kwenye mazoezi.

Lamine alikuwa kwenye sehemu ya kikosi cha kwanza cha Yanga msimu uliopita huku akiwa mmoja kati ya wachezaji wa kimataifa waliobaki kikosini sambamba na kipa Farouk Shikhalo na kiungo Haruna Niyonzima.

Beki huyo hakuwa pia kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir uliochezwa uwanja wa Mkapa katika siku ya kuhitimisha kilele cha wiki ya wananchi hivyo nafasi yake alicheza Mwamnyeto na timu yake ikaibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala