Connect with us

Makala

La Liga Kuanza Rasmi Mazoezi Jumatatu

Wakati England na baadhi ya timu zikianza mazoezi kwa ajili ya kuangalia mustakabali wa kuendelea kwa msimu huu, timu za Hispania zikiwemo Madrid na Barcelona zenyewe mazoezi zitaanza Jumatatu ijayo.

Waziri Mkuu wa Hispania, Pedro Sanchez ametangaza kuwa Jumatatu ijayo ya Mei 4 mwaka huu timu zitaanza mazoezi huku wakiendelea kujikinga dhidi ya corona.

Ligi mbalimbali duniani zimesimama kutokana na corona ambapo La Liga inatarajiwa kuendelea Mei, mwaka huu halikadhalika Bundesliga  kama ilivyo kwa Premier.

Tayari Ufaransa imeshafuta msimu huu pamoja na Uholanzi kutokana na janga hilo la corona na kabla ya kufikia uamuzi huo serikali zao zilitangaza kusimamisha masuala ya michezo hadi Septemba mwaka huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala