Connect with us

Makala

Kwaheri Tshishimbi

Kiungo wa klabu ya Yanga Papy Tshishimbi ameondoka kwao Congo kuangalia familia yake ndugu na jamaa zake ambao hawajaonana kwa kipindi kirefu tangu aje Tanzania na kutumikia kikosi hicho.

Mkongomani huyo alimuaga kocha mpya Luc Eymael siku moja kabla ya kuanza mazoezi nao kuwa ana matatizo ya kifamilia hivyo inabidi aelekee kwao Congo ila atawahi kurudi kabla ya mchezo wao dhidi ya Azam Fc siku ya Jumapili.

“Sikupanga kurudi nyumbani kwa kipindi hiki lakini imenilazimu kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu ,lakini nitawahi kurudi haraka sitaki kukosa mechi ya Azam pia sijahudhuria mazoezi ya kocha wetu mpya tangu ameanza”alisema Tshishimbi ikiwa na familia yake ipo salama kwa sasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala