Connect with us

Makala

Kurejea Yondani,Shikalo Roho Kwatu

Kipa wa Yanga Mkenya Farouk Shikalo amefurahishwa na kurejea kwa beki mkongwe Kelvin Yondani ambaye aligoma kujiunga na kambi ya timu hiyo baada ya kutokamilishiwa baadhi ya madai yake ya fedha na klabu hiyo.

Beki huyo amejiunga na kambi hiyo iliyopo mkoani Kilimanjaro ambapo wanajiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Fc na Afc Leopard kabla ya kuwavaa Township Rollers nchini Botswana.

Kelvin Yondani

Farouk amefurahishwa na ujio wa beki huyo kutokana na uimara aliokua nao kukabana na washambuliaji wakorofi akikumbuka alivyomkaba Michael Olunga wa kenya wakati timu hizo zilipokutana katika michuano ya Afcon nchini Misri.

“Ni beki mzuri na mzoefu,imenichukua dakika tano tu mazoezi kubaini uimara wake”alisema Shikalo

Yanga inakabiliwa na mchezo muhimu dhidi ya Rollers baada ya mechi ya awali iliyofanyika jijini kuisha kwa sare ya moja kwa moja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala