Dakika ya 68 wakati mechi ya Tanzania na Algeria ikiendelea baada ya Boko kuokoa mpira na ukamkuta dogo mmoja hatari aliayeachia shuti kali na kumuacha kipa Aishi Manula asijue la kufanya na kuipa ushindi timu yake ya Senegali katika michuano ya Afcon.
Huyo ni Krepin Santos Diatta kiungo wa kushoto wa senegali aliyezaliwa 25 february 1999 yaani ana miaka 20 tu mpaka jana wakati anaiua Stars kwa shuti la mtu mzima.
Krepin mwenye urefu wa futi 5 na inchi 8 ana uzito wa kilo 68 zinazomfanya kuwa mnyambulifu na kusababisha usumbufu mkubwa kwa mabeki huku silaha ya kubwa ikiwa ni mguu wake wa kulia anaoutumia vyema katika nafasi ya kiungo upande wa kushoto mwa uwanja.
![](http://sportsleosw.com/wp-content/uploads/2019/06/4442012-300x168.jpg)
Krepin alianzia maisha ya soka katika akademia ya Oslo nchini Norway na baadae alijiunga na timu ya Sarpsborg aliyodumu naya kwa mwaka mmoja akiichezea michezo 22 na kufunga mabao 3 na baadaye januari 2018 alijiunga na Club Brugge ya Ubelgiji kwa mkataba mrefu mpaka mwaka 2022 kwa dau la Euro 2m.
Mpaka sasa amecheza michezo 59 katika ngazi ya vilabu na kufunga magoli matano na aliitwa timu ya taifa ya vijana kwa mara ya kwanza 2016 na kufanikiwa kuichezea michezo 19 na kufunga mabao 7 akiisaidia timu hiyo kumaliza nafsi ya pili katika michuano ya Afcon ya vijana nchini Zambia.
![](http://sportsleosw.com/wp-content/uploads/2019/06/56490510_131894777900202_1756802207987266280_n-240x300.jpg)
Kwa upande wa timu ya taifa ya Senegal ya wakubwa aliitwa kwa mara ya kwanza mwaka huu mwezi february katika maandalizi ya mchezo wa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika dhidi ya Madagascar na kocha Cisse.
Mchezo wa jana dhidi ya Tanzania ulikua ni mchezo wa pili wa kinda huyo na alifanikiwa kufunga goli moja na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi hiyo.
Timu kubwa mbalimbali barani ulaya zimekua zikimuangalia kinda huyu kwa ajili ya kumsajili huku ikadaiwa mwaka 2017 kocha wa Manchester united Jose Mourinho aliwaagiza wasaidizi wake kumfatilia staa huyo.