Connect with us

Makala

Kocha Simba Hakutegemea Kupata Zero

Kocha mkuu wa Simba Sc ,Sven Vandenbroeck hajategemea kama angeliweza kupoteza kwenye mchezo dhidi ya Yanga kwa jinsi kikosi chake kilivyoweza kujiandaa vyema na kufanya maandalizi ya kuweza kunyakua ubingwa huo.

Sven amekabidhiwa kikosi kikiwa na rekodi ya kuifunga Yanga kwa miaka minne lakini Eymael ambae ni kocha mkuu wa Yanga kwa sasa ameivunja rekodi hiyo na kuifunga simba ambayo makocha wengine wameshindwa.

“Bahati mbaya sana kwangu kupoteza mechi ya ndani dhidi ya Yanga kwani ni rekodi ambayo iliwekwa miaka minne nyuma timu yangu kutopoteza”alisema Sven.

Aliongeza kwa kusema ,tumejifunza vitu vingi katika mchezo huu baada ya kupoteza na tutakwenda kuvitumia katika mechi zijazo ili kushinda.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala