Connect with us

Makala

Kocha Ndanda Aingiwa Na Wasiwasi

Abdul Mingange ambaye ni kocha mkuu wa Ndanda FC amesema kuwa kusimamishwa kwa ligi kuu bara kwa muda wa mwezi mmoja kutawatoa wachezaji wake kwenye reli kutokana na kasi waliyoanza kuitengeneza.

Kikosi hiko kilikuwa kimerejea kwenye ubora wake ambapo kwa mwezi Februari Mingange aliingia kwenye kuwania tuzo ya kocha bora wa mwezi huku mchezaji wake Vitalis Mayanga akiibuka mchezaji bora wa mwezi Februari.

Mingange amesema kuwa kusimamishwa kwa ligi kwa sababu ya kupambana na Virusi vya Corona ni jambo la msingi kutokana na umuhimu wa afya lakini ana wasiwasi mkubwa na vijana wake kutoweza kurejea kwenye kasi ambayo walianza kuwa nayo.

Ndanda Fc inashika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 31 katika mechi 29 alizocheza huku akitoa sare 10 na kushinda mechi 7 huku akipoteza mechi 12.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala