Connect with us

Makala

Kisa Corona,Wachezaji Wapata Hofu

Mshambuliaji wa Manchester City nchini Uingereza, Sergio Aguero amesema kuwa wanahofia kurejea uwanjani  wakati huu ambapo janga la Covid-19 halijadhibitiwa vilivyo takribani mataifa yote duniani .

Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ilitarajiwa kuendelezwa mnamo Juni 8 hali ambayo ingehitaji wachezaji kurudi mazoezini kikamilifu kufikia Mei 18.

Vinara wa vikosi vyote 20 vya EPL wanatazamiwa kukutana leo Ijumaa ya Mei 1, 2020 kujadili njia mbalimbali za kurejelewa kwa kampeni za muhula huu .

“Wachezaji wengi wanaogopa kurejea uwanjani kwa sababu wana watoto na familia ambazo zinawategemea pakubwa” alisema Aguero, wakati akihojiwa na runinga ya El Chiringuito nchini Argentina.

Nyota huyo mwenye kuzifumania nyavu aliongeza  kuwa wachezaji wengi wanasema kuna watu walio na virusi vya corona ila hawaonyeshi dalili zozote za ugonjwa huo hivyo itakuwa rahisi sana kwa watu kuambukizana iwapo watarejea uwanjani ikiwa hali si shwari.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala