Connect with us

Makala

Kapombe Hatihati Afcon

Beki wa Simba sc Shomari Kapombe ana hatihati ya kutokwenda katika michuano ya mataifa ya Afrika(Afcon) baada ya kutopona majeraha yake kwa asilimia 100.Kapombe aliyeumia katika kambi ya siku kumi nchini Afrika kusini wakati taifa stars ikijiandaa na mechi ya kuwania kufuzu fainali hizo dhidi ya Lesotho mechi ambayo stars ililala kwa goli moja bila.

Licha ya kupata matibabu nchini Afrika kusini,Kapombe amekua nje ya uwanja kwa muda mrefu na hivi sasa alikua tayari ameshaanza mazoezi kabla ya kujitonesha jeraha lake hilo katika kambi ya taifa stars iliyoko hoteli ya White Sands.

Kapombe amekua chini ya uangalizi wa madaktari wa Taifa stars wakishirikiana na wale wa simba kuhakikisha anarejea na utimamu wake ili kuweza kutumika katika michuano hiyo itakayofanyika nchini misri ambapo stars itatupa karata yake ya kwanza june 23 dhidi ya Senegal.

Hata hivyo kama atashindwa kurudisha utimamu wake,beki huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi za ulinzi zote pamoja na kiungo hatakuwamo katika orodha ya wachezaji watakaotumika katika michuano hiyo ambayo stars imefuzo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980.

Stars imepangwa kundi c na timu za Senegal,Algeria na majirani zetu wa Kenya na itamaliza mechi za makundi julai 1 kwa kucheza na Kenya

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala