Beki wa klabu ya Simba Shomari Kapombe amekanusha taarifa zilizosambaa zikidai ametonesha majeraha yake wakati akifanya mazoezi na kikosi cha timu ya taifa kinachojiandaa na michuano ya Afrika (Afcon),Beki huyo mwenye uwezo wa kucheza kwa ufasaha nafasi zote za ulinzi na ile ya kiungo amekanusha taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii.
Katika taarifa iliyotolewa na akaunti ya mchezaji huyo kupitia mtandaa wa instagram ameonyesha kusikitishwa kwake na taarifa hizo huku akisisitiza kuwa yupo salama na hajajiunga na timu ya taifa kwa sababu ana programu maalumu aliyoachiwa na kocha wa viungo wa simba kwa ajili ya kurejesha utimamamu wa mwili.Taarifa aliyoitoa Kapombe ilisomeka kama ifuatavyo.
“Ni jambo la kusikitisha na linaloumiza kwa kias kikubw kwa taarif hii inayoendelea kusambazwa na vyomb vya habari na watu mbalimbali kuwa nimeumia /nimejitonesha jerah langu hakika hz habari sio za kweli kabisa na hazina uhakika na ukweli wwt, katika siku niliyoumia ni leo najiuliza nitaumiaje nikiwa nipo nyumb na camp cjaingia au kufanya mazoez na timu ya taifa??? mm niko mzima na nafanya mazoezi yang vzr nafuata program yng niliyoachiwa na fitness coach wangu wa Simba . Mm pamajo na familia yangu tumeumizwa na taarifa hii ni kubwa na nzito kwet naomba vyombo vya habari kutoa taarifa iliyokuwa sahih na yenye ukweli wa asilimia mia. Wanasimba na watanzania wote, wapenda soka napenda kuwaambia kuwa mimi niko sawa na hakuna ukweli wwt kuhus mimi kuumia tena hz taarifa sio sahihi kwa wote waliyotoa taarifa hz au kusambaza….Mungu nipe uvumilivu na haya yatapita🙏🙏🙏🙏🙏 “.