Connect with us

Makala

Jezi Ziandaliwe-Manchester United

Ligi Kuu ya England inaweza kurejea Juni 8 ambapo kutakuwa na maandalizi mafupi ya muda wa wiki tatu kwa timu kushiriki na wachezaji pia watawekwa karantini kabla ya kuanza kucheza ili kuona kama wana maambukizi ya Corona.

Wachezaji wa timu ya Manchester United wameambiwa kuwa wanatakiwa kuanza kujifulia nguo zao wenyewe kuelekea kurejea kwa mazoezi Mei 18 baada ya ligi kuu ya England kusimamishwa kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Maamuzi ya kutakiwa kuosha na kufua vifaa vyao vya mazoezini ni kwa sababu hakutakuwa na huduma hiyo kwa kipindi cha hivi karibuni na wale wachezaji waliosafiri nje ya England wanapaswa kujitenga Siku 14 pale watakaporejea ili kuona kama wana maambukizi ya virusi hivyo.

Pia wachezaji hao wametakwa kutumia usafiri binafsi wanapokwenda mazoezini uwanja wa Carrington na kuoga kwenye mabafu yao ya  nyumbani.

Manchester United ipo nafasi tano Kwenye msimamo wa ligi kuu England ikiwa na pointi zake 45 baada ya kucheza mechi 29.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala