Connect with us

Makala

Jarida La Yanga Kutangazwa Rasmi

Uongozi wa klabu ya Yanga chini ya Mwenyekiti Dk.Mshindo Msolla,umeandaa jarida maalumu ambalo litakuwa linahusu mambo mbalimbali ya klabu .

Jarida hilo lilizinduliwa Aprili 30 lenye kurasa 48 linalouzwa kwa bei ya shilingi 5000 nchini kote kupitia matawi mbalimbali ya Yanga Sc.

Msolla amesema kuwa jarida hilo limetengenezwa kwa ajili ya mashabiki wa timu hiyo ili kusoma na kufahamu mambo mbalimbali yanayoihusu timu hiyo pia limeambatana na neema kwa mashabiki ambao watanunua jezi za timu hiyo katika maduka ya GSM, watalipata jarida hilo bure.
“Jarida letu hili tumeliandaa kwa ajili ya kuwaelimisha mashabiki wetu mambo mbalimbali yaliyotokea zamani na sasa ambapo jarida hili litapatikana kwa Sh 5000 tu ila kwa wale ambao watanunua jezi za Yanga katika maduka ya GSM watalipata jarida hili bure kabisa” alisema Msolla

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala