Connect with us

Makala

Ighalo Awasubiri Spurs

Mshambuliaji Odion Ighalo amesema kikosi cha sasa cha Manchester United kipo katika hali nzuri tayari kwa msimu wa ligi ya EPL kikisubiri kwa hamu mechi hizo kurejewa .

Michuano ya ligi hiyo Kuu ya Uingereza (EPL) zitarejelewa katikati mwa juma lijalo ambapo United wataanza na Tottenham Hotspur Ijumaa, katika mechi ambayo Ighalo anatarajia timu yake kung’ara. Ighalo ambaye mkataba wake ulitarajiwa kumalizika mwaka huu alikubali mkataba mpya ambao utamalizika Januari 2021 .

“Nitaendelea kuweka bidii mazoezini, huku nikilenga kuvuma zaidi katika mechi za usoni,” aliwaambia waandishi kupitia kwa mtandao rasmi wa klabu hiyo ya Old Trafford .

“Nimeimarika kwa kiasi kikubwa baada ya kufanya mazoezi makali ya wiki mbili. Najisikia kuwa katika hali nzuri ya kung’ara mechini iwapo nitapewa nafasi kikosini. Nangojea kwa hamu mechi ya Ijumaa dhidi ya Spurs.”

Cc:Dominick Salamba

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala