Connect with us

Makala

Gwambina Waipiga 2-0 Ihefa Fc

Gwambina FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ihefa Fc katika mchezo wa leo wa raundi ya tano ligi kuu bara msimu  2020/2021.

Mchezo huo ulichezwa uwanja wa CCM Kirumba baada ya Uwanja wa Gwambina Complex kufungiwa na bodi ya ligi Tanzania kwa kuwa haujakidhi vigezo.

Mabao yote ya Gwambina FC yamepachikwa nyavuni mwa Ihefa na Meshack Abraham dakika ya 33 na 48 huku wakinyakua pointi tatu muhimu na kuwafanya Ihefu wapoteze alama hizo kwenye mzunguko wa tano.

Gwambina inafikisha jumla ya pointi nne kibindoni kwa mara ya kwanza baada ya kupoteza raundi nne zilizopita huku Ihefu ikibakiwa na pointi tatu kwa kuwa ilishinda mchezo mmoja mbele ya Ruvu Shooting.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala