Connect with us

Makala

Furaha Azam Festival,Mabao 2-1

Azam Fc imewachapa mabao 2-1 Namungo Fc katika sikukuu yao ambayo ilihudhuriwa na umati wa mashabiki katika uwanja wao wa Chamazi,Azam Complex.

Azam Festival imehudhuliwa na wasanii wakubwa maarufu mmoja akiwa ni muimba bongofleva ambaye ni Alikiba(King Kiba)huku mwingine akiwa ni Msagasumu ambaye ni msanii wa singeli.

Bao la kwanza la Azam Fc lilipachikwa langoni mwa Namungo dakika ya 37 na Obrey Chirwa huku la pili likifungwa na Andrew Simchimba dakika ya 66.

Bao la kufutia machozi kwa upande wa Namungo Fc lilifungwa na Stephen Sey dakika ya 58.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala