Connect with us

Makala

Frank De Boer Apewa Mikoba Ya Koeman

Kocha wa zamani wa Ajax,Frank De Boer ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uholanzi kwa ajili ya kujaza pengo lililoachwa na Ronald Koeman ambaye kwa sasa anainoa Barcelona baada ya Quique Setien kuvuliwa mikoba hiyo kutokana na matokeo duni.

De Boer ambaye pia aliwahi kuwa beki wa Ajax na Barcelona amepewa kandarasi ya miaka miwili kuitumikia timu hiyo ambao utatamatika mwishoni mwa fainali za kombe la Dunia zitakazoandaliwa nchini Qatar mwaka 2022.

Mchuano wa kwanza kwa De Boer kusimamia kambini mwa Uholanzi ni ule wa kirafiki utakaowakutanisha na Mexico jijini Amsterdam Octoba 7,2020 kabla ya kuwaongoza vijana wake kuvaana na Bosnia-Herzegovina na Italia katika UEFA Nations League Octoba 11 na 14 mwaka huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala