Connect with us

Makala

Fraga Wa Simba Ampa Tano Bwalya

Gerson Fraga Vieira wa Simba Sc ambaye pia ni raia wa Brazil ameufurahia usajili wa kiungo kutoka Lusaka Dynamosi iliyoko Zambia,Larry Bwalya kutokea kwani ni miongoni mwa usajili bora ambao umefanyika.

Kiungo huyo amesema kuwa uwezo anaouonyesha Bwalya katika viwanja vya mazoezi vya Simba Mo Arena vilivyoko Bunju jijini Dar ni mkubwa kwani anafarijika sana kuwepo upande wake kwakuwa amekuwa kipenzi cha mashabiki kwa mda mfupi hasa alipotoa pasi katika mchezo wa Simba day ambapo walipambana na Vital’O’ wa Burundi na kuwafunga mabao 6-0.

Fraga pia amekuwa miongoni mwa viungo waliofanya vizuri katika msimu uliopita akiwa na kiungo mwenzake Deo Kanda raia wa Congo ambaye msimu huu sio miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Simba kwa kuwa hakuongezewa mkataba.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala