Connect with us

Makala

Fernandes Aaga Kwa Kilio

Nahodha wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes ameangua kilio wakati akiicheza timu hiyo mechi ya mwisho dhidi ya Valencia akijiandaa kukamilisha uhamisho wake kujiunga na Manchester united kwa thamani ya paundi milioni 56.

Bruno Fernandes (kulia)akifuta machozi wakati timu zikikaguliwa.

Kiungo alifunga mabao 32 na kusaidia upatikanaji wa mengine 18 katika michezo 51 ya timu yake anajiandaa kusafiri kwenda jijini Manchester kukamilisha usajili huo na vipimo vya afya.

Fernandes alitoa machozi akiwa kwenye benchi la timu hiyo hali iliyoashiria kuwaaga wachezaji wenzake na benchi la ufundi kujiunga na mashetani wekundu baada ya tetesi za kumuhitaji kwa muda mrefu kuzagaa.

Licha ya kuivutia United kiungo huyo pia amezivutia klabu kadhaa barani humo kama Liverpool,Man city,Paris st.German kutokana na rekodi zake za msimu uliopita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala