Connect with us

Makala

Farid Aanza Kujinoa Leo Yanga

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Farid Mussa ameanza mazoezi rasmi leo Agosti 19 na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na mechi nyingine za ushindani za msimu wa 2020/2021.

Farid amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Yanga Sc akitokea kwenye klabu ya CD Tennerife kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake.

Yanga ilianza mazoezi Agosti 10 mapema kabisa kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria na mchezo wao wa kwanza  ndani ya ligi kuu bara utakuwa dhidi ya Tanzania Prisons katika uwanja wa Mkapa, Septemba 6.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala