Connect with us

Makala

Eti Tyson Haogopi Kifo

Bingwa wa zamani wa Ndondi mwenye uzito mkubwa duniani ,Mike Tyson ameeleza kuwa anasubiri kwa hamu kifo chake kwani kuishi kunaweza kuwa na gharama kubwa kuliko kufa.

Tyson anashikilia rekodi ya bingwa wa uzito mkubwa duniani mwenye umri mdogo zaidi alipomtwanga Trevor Berbick kwa knockout mwaka 1986 akiwa na umri wa miaka 20.

Bingwa huyo mwenye miaka 53 kwa sasa amesema kutoogopa kwake jambo lolote kulimfanya awe tayari kwa kifo ulingoni japo aliamini ndiye ambaye angeua endapo kungetokea kifo katika moja ya mapambano yake.

Kwa sasa maisha ya mwanandondi huyo yamekuwa magumu tofauti na umaarufu aliokuwa nao zamani ,hii ni baada ya  kustaafu ndondi na maisha yake yalibadilika tangu afungwe jela miaka 3 baada ya kubainika ana hatia ya ubakaji.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala