Connect with us

Makala

Epl Washirikisha Polisi Kutoa Mawazo

Kundi la vilabu vya ligi kuu vimepanga kufanya mazungumzo na vikosi vyao vya polisi wiki hii kwa matumaini ya kuwa wazo la kutumia viwanja ambavyo ni tofauti na viwanja vyao (Neutral Venues) linaweza kubatilishwa.

Vilabu kadhaa vinaamini kuwa vikosi vyao vya Polisi  pamoja na kikundi vyao vya ushauri wa usalama, ambavyo huwa vinatoa ruhusa ya usalama na kuridhia kuchezwa kwa mechi vitathibitisha kuwa viko tayari kusimamia mechi za nyumbani ili tu kuwepo na mtindo wa nyumbani na ugenini na sio kutumia viwanja tofauti na vyao pindi ligi itakapo rejea .

Hata hivyo Premier League wanafikiria kubadili maamuzi ya vilabu kutumia viwanja tofauti na badala yake watumie viwanja vyao kama kawaida(usual stadium)ikiwa na maana kuwa kutakuwa na nyumbani na ugenini.

Ikumbukwe kuwa vilabu vya Aston Villa, Brighton, na vingine vilivyopo chini ya msimamo wa ligi kuu England ni miongoni mwa vilabu vinavyopinga vikali wazo la kutumia viwanja tofauti na vyao (Neutral Venues) .

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala