Connect with us

Makala

Chama Akabidhi Milioni Moja Kwa Yatima Leo.

Clatous Chama wa Simba Sc amekabidhi msaada wa Tsh milioni 1 katika kituo cha watoto yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekeleza wa ahadi yake aliyoitoa jana Agosti 3 wakati anakabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa Simba iliyotolewa na mdhamini mkuu wa kampuni ya Sportpesa.

Chama amekuwa kinara ndani ya Simba baada ya kutengeneza jumla ya pasi 10 na kufunga mabao mawili akiwa chini ya kocha mkuu Sven Vandenbroeck.

Kikosi chake kimetwaa mataji matatu msimu wa 2019/20 ikiwa ni pamoja na ngao ya jamii, taji la ligi kuu bara na kombe la shirikisho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala