Connect with us

Makala

Borussia Dortmund Wapata Mrithi Wa Lewandowsk

Katika ufunguzi wa dirisha la usajili mdogo mwezi huu Januari tetesi nyingi zimesikika za usajili unaomhusu Erling Haaland ambaye anaitumikia Red Bull Salzburg.

Erling Haaland ni mchezaji bora wa kufunga mabao kwa kujua wapi asimame aweze kutupia mpira nyavuni ameongeza thamani kwa kuwa straika chipukizi mwenye ubora mkubwa hata kuwindwa na vigogo wa Ulaya.

Iliaminika kuwa ukaribu alionao mchezaji huyo na Manchester United itamsajili lakini Borussia Dortmund inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’ iliibuka na kumsajili Haaland kama mchezaji wao.

Borussia Dortmund inaamini wamefanya chaguo la pekee kumsajili mchezaji huyo kwani ataweza kufiti mfumo wa timu hiyo kama ilivyokuwa kwa Robert Lewandowsk japo imepita miaka sita tangu mchezaji huyo ahamie timu pinzani Bayernn Munich na hakupatikana wa kumfiti.

Marcos anaamini sasa namba tisa mpya Erling Haaland anaweza kufiti vizuri mfumo wao na Bundesliga itanogeshwa kama enzi za Robert Lewandowsk.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala