Home Soka Bocco Rasmi Jkt Tanzania

Bocco Rasmi Jkt Tanzania

by Sports Leo
0 comments

Baada ya Klabu ya Simba kutangaza kuachana na John Bocco kama mchezaji wa kikosi chao katika msimu mpya wa 2024/25 huku ikitangaza kumpa mikoba ya kuwa kocha mkuu wa Kikosi cha Vijana wa Umri chini ya miaka 17 wa klabu ya Simba,Staa huyo rasmi ametambulishwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Jkt Tanzania kwa ajili ya msimu ujao.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ameonekana akifanya mazoezi kwenye uwanja wa Meja Generali Isamuhyo akiwa na uzi wa JKT Tanzania tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25 akiwa kama mchezaji mpya wa kikosi hicho.

banner

Bocco aliyedumu Simba sc kwa miaka saba amejiunga na Jkt kama mshambuliaji mpya kuongeza nguvu kikosini humo na tayari ameshaanza mazoezi na klabu hiyo.

Pamoja na majukumu ya uchezaji pia mshambuliaji huyo atakua anasaidiana na benchi la ufundi katika mambo mbalimbali ya kiufundi kutokana na kuwa na uzoefu wa kutosha baada ya kucheza mpira kwa takribani miaka 16 hapa nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited