Connect with us

Makala

Bocco Chaguo Namba Moja Kwa Sven

Kocha mkuu wa Simba Sc, Sven Vandenbroeck amemtangaza John Bocco kama nahodha wa timu hiyo na chaguo lake katika kikosi chake cha kwanza katika msimu mpya wa ligi kuu bara 2020/2021.

Meddie Kagere anaikosa nafasi hiyo licha ya kuwa mfungaji bora mara mbili mfululizo katika misimu miwili iliyopita ambayo ni ya 2018/2019 ambapo alipachika mabao 23 na 2019/2020 ambapo pia alipachika mabao 22 pekee.

Sven anamchagua Bocco kama nahodha wa kikosi hicho kutokana na kiwango chake bado ni kizuri na aina ya mifumo anayoitumia katika soka pia inamfurahisha hivyo haoni sababu ya kumuweka benchi na kumpanga mchezaji mwingine.

“Ninaamini uwezo wa washambuliaji wangu wote waliokuwepo katika timu, lakini mara nyingi nimekuwa nikimpa nafasi mchezaji yule aliye kwenye kiwango bora katika timu hasa Bocco anayetimiza majukumu yake vizuri ikiwemo kucheza kwa kufuata maelekezo”alisema Sven

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala