Connect with us

Makala

Balinya Atua Gormahia

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Juma Balinya amesajiliwa na timu ya Gor Mahia, mabingwa wa ligi kuu ya Kenya.

Gor Mahia imemsajili Balinya baada ya kujiridhisha na uwezo wake hasa baada ya kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uganda kwa msimu uliopita.

Balinya aliyekuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uganda, awali alisajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na kutambulishwa kwa mbwembwe wakati wa kilele cha siku ya wiki ya mwananchi jijini Dar es salaam.

Hata hivyo alidumu Yanga kwa miezi sita tu, kabla ya makubaliano ya kuvunja mkataba baina yake na Yanga kufikiwa.

Nyota huyo ni kama amepishana na Yikpe Gnamien aliyesajiliwa na Yanga akitokea Gor Mahia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala