Connect with us

Makala

Azam Fc Yawasili Bukoba Kuivaa Kagera Sugar

Msafara wa kikosi cha timu ya Azam Fc tayari umewasili mjini Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Kagera Sugar Fc utakaofanyika siku ya Jumamosi April 19 2025.

Msafara wa kikosi hicho umewasili salama mchana wa leo ambapo watafanya mazoezi mepesi kisha kesho watapata nafasi ya kufanya mazoezi katika uwanja wa Kaitaba utakaofanyika mchezo huo.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na ubora wa siku za karibuni wa kikosi cha Kagera sugar tangu Kocha Juma Kaseja achukue timu hiyo.

Kocha Rachid Taoussi ana kazi ya ziada kuchukua alama tatu katika mchezo huo baada ya kufungwa 2-1 na Yanga sc katika mchezo uliopita nyumbani Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.

Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Azam Fc ipo nafasi ya tatu na alama 51 huku Kagera Sugar ipo nafasi ya 15 ikiwa na alama 22 katika michezo 26 ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala